Bitcoin
Tuesday, January 29, 2013
Monday, January 28, 2013
PICHA ZA LULU NA MAELEZO YA MASHARTI JUU YA DHAMANA YAKE LEO JAN 28
Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Saturday, January 12, 2013
Saturday, January 5, 2013
VIDEO YA P.UNIT ILIYOFUNGIWA CITIZEN TV KENYA.
Hii ndio video ya P Unit ft Collo ‘you guy’ iliyofungiwa na kituo maarufu cha Tv nchini Kenya cha CITIZEN baada ya kuonekana kwamba picha zake zimekaa kingono zaidi na haziwezi kuonyeshwa kwenye Tv hiyo ambayo ina mamilioni ya mashabiki wa kila rika kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla.
Video ya ‘You Guy’ ambayo P Unit wametumia mamilioni kuitengeneza kupitia kwa producer maarufu wa Nigeria ambae amewahikufanya kazi na mastaa kibao wakiwemo P Square haina hata mwezi mmoja toka itoke, pamoja na kwamba imefungiwa kuonyeshwa CITIZEN TV bado inaendelea kupigwa kwenye vituo vingine.
Subscribe to:
Posts (Atom)